Bunge latoa ufafanuzi kuhusu wabunge waliotimuliwa CUF
Akitoa ufafanuzi huo kwenye ofisi za Bunge Dodoma Kagaigai anasema mahakama imetoa uamuzi wa awali juu ya walalamikiwa wa shauri la wabunge hao ambao ni baraza la wadhamini na uongozi wa CUF kuwa wasitishe utekelezaji wa kuwafukuza uanachama na kutojadili uanachama wao hadi mahakama itakaposikiliza shauri lao la msingi.
Aidha Kagaigai amesema nafasi za ubunge hao tayari zilijazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria, na wabunge waliopatikana kujaza nafasi hizo wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya kibunge ipasavyo.
Novemba 10,mwaka huu mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam ilitoa uamuzi wa awali katika shauri namba 479 la mwaka 2017 lililofunguliwa na waliokuwa wabunge nane wa CUF viti maalum uliotafsiriwa tofauti na baadhi ya watu kwa kudhani wabunge hao wamerejeshewa uanachama wao na hivyo wanarudi katika nafasi zao za ubunge.
Bunge latoa ufafanuzi kuhusu wabunge waliotimuliwa CUF
Reviewed by Zero Degree
on
11/30/2017 06:50:00 PM
Rating: