Loading...

Matola amfungulia milango Asante Kwasi

Kocha wa Lipuli FC, Suleiman Matola
KOCHA wa Lipuli FC, Suleiman Matola "Veron", amewaambia Simba kama wanamtaka beki wake wa kati Mghana, Asante Kwasi, kwenda kukamilisha mazungumzo haraka kwa sababu anajua atawasaidia kwenye mashindano ya kimataifa mwakani.

Kwasi ambaye alitua Lipuli akitokea Mbao FC ya Mwanza, alionyesha uwezo mzuri na kufanikiwa kuisawazishia timu yake bao katika mechi iliyochezwa Jumapili dhidi ya Simba wanaodhaminiwa na Kampuni ya SportPesa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Nipashe, Matola alisema kuwa, hata kama Simba itafanikiwa kumchukua beki huyo, kikosi chake hakitakuwa na pengo kwa sababu wapo mabeki wengine ambao wana uwezo na uzoefu wa kukabiliana na ushindani wa mechi za Ligi Kuu.

"Kama kweli Simba wanania ya kumsajilibeki wetu, waje rasmi, na akiondoka sitakuwa na pengo kubwa kwa sababu tunaye Lufunga (Novalty) na Martine (Kazila) ambao ni wazuri na walishafanya vyema wakati Asante Kwasi akiwa majeruhi na alikosa mechi kadhaa za awali," alisema Matola.

Kiungo na nahodha huyo wa zamani wa Simba alisema pia katika dirisha dogo anahitaji kuboresha kikosi chake katika safu ya ushambuliaji na tayari ameshawasilisha barua kwa Wekundu wa Msimbazi akiwahitaji Juma Luizio na Jamal Mnyate.

Kwasi ana mkataba wa mwaka mmoja na Lipuli utakaomalizika mwakani na tayari ameshaanza mazungumzo ya chini kwa chini na Simba kwa ajili ya kujiunga nayo kwenye kipindi cha dirisha dogo.

Lipuli FC, Njombe Mji FC na Singida United ambayo iko katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ndio timu tatu zilizopanda daraja msimu huu.
Matola amfungulia milango Asante Kwasi Matola amfungulia milango Asante Kwasi Reviewed by Zero Degree on 11/30/2017 07:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.