Loading...

CHADEMA waiomba serikali kuruhusu mikutano ya Siasa


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mheshimiwa FREEMAN MBOWE ameitaka serikali kubadili uamuzi wa kuzuia mikutano na shughuli nyingine za siasa kwa kuwa Tanzania ilishakubali na kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA],  Freemn Mbowe
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wake wa kumnadi mgombea wa udiwani katika Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa, Mheshimiwa MBOWE amesema serikali iliyopo madarakani imechaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano hivyo inapaswa kuheshimu sheria pamoja na katiba hiyo ikiwemo sheria namba tano iliyorejesha mfumo huo mwaka 1992 kabla ya hapo awali kufutwa mwaka 1965.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji PETER MSIGWA amewataka wananchi wa Kata ya Kitwiru kuchagua mgombea wa CHADEMA ili aongeze nguvu kwenye baraza la madiwani linaloongozwa na chama hicho ambalo limeifanya Manispaa ya Iringa kuwa mfano wa kuigwa katika mambo mengi ya uendeshaji halmashauri nchini.

Kwa upande wake Mgombea wa udiwani kupitia chama hicho,Bwana BAHATI CHENGULA amewataka wananchi kuendelea kumwamini kama walivyomwamini awali na kumchagua kuwa Mwenyekiti wa mtaa ,kazi ambayo ameifanya kwa uadilifu na kujituma kwa lengo la kusukuma mbele maendeleo yao.
CHADEMA waiomba serikali kuruhusu mikutano ya Siasa CHADEMA waiomba serikali kuruhusu mikutano ya Siasa Reviewed by Zero Degree on 11/18/2017 09:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.