Loading...

Uamuzi wa Conte kuhusiana na suala la David Luiz

David Luiz
Antonio Conte amethibitisha kwamba, David Luiz atarejea kwenye kikosi cha Chelsea kitakachocheza dhidi ya West Brom.

Mbrazil huyo aliachwa nje ya kikosi kilichoibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester United baada ya kukosoa mbinu alizotumia kocha wake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma uliomalizika kwa Chelsea kuchapwa goli 3-0.

Kwa mujibu wa taarifa ya 'Mirror', Conte alisema kwamba lilikuwa ni tatizo dogo tu la kiufundi na ana panga kumrejesha Luiz kikosini kwa ajili ya mechi yao dhidi ya West Brom.

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte
"Yumo ndani ya kikosi. Ilikuwa ni maamuzi ya kiufundi na kila mchezaji anatakiwa kulitegemea hilo na kukubaliana na uamuzi," alisema.

"Hili ni jambo la kawaida. Sipendelei kujadili kuhusu mchezaji mmoja pekee.”

Kwa kiwango alichokionyesha Andreas Christensen kwenye mechi dhidi ya Manchester United ni dhahiri kabisa kwamba uwezekano wa Luiz kuanza na kikosi cha kwanza ni mdogo sana.

Conte aliongeza: "Msimu huu ni mzuri kwetu sote, kwa Christensen, hata kwangu pia, kwani nina nafasi nzuri.

“Anaonyesha kuwa ni mchezaji mzuri. Anacheza kama mtu mzima na nina imani ataendelea kukua katika kiwango hicho na pengine zaidi ya hapo.”

Conte pia alizungumzia suala la kujiuzulu kwa mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo, Michael Emenalo.

"Kwa hakika ni pigo kubwa kwetu. Uhusiano wangu na Michael ulikuwa mzuri sana, alinisaidia sana msimu huu," aliongeza.

"Wakati huo huo, tunatakiwa kuheshimu uamuzi wake. Namtakia yeye na familia yake maisha mema sasa na kwa wakati ujao.”
Uamuzi wa Conte kuhusiana na suala la David Luiz Uamuzi wa Conte kuhusiana na suala la David Luiz Reviewed by Zero Degree on 11/18/2017 02:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.