Loading...

Chelsea, Manchester United kuwania saini ya straika mwenye thamani ya paundi milioni 89


Kwa mujibu wa taarifa ya 'Daily Mirror', Klabu za Chelsea na Manchester United zinatarajiwa kuingia kwenye ushindani mkubwa kuwania saini ya mshambuliaji wa Italia, Andrea Belotti anayeichezea klabu ya Torino.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kuondoka Torino mwishoni mwa msimu huu na anawindwa na klabu kubwa za barani Ulaya, ikiwa tayari Real Madrid pia wameonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Mshambuliaji wa Torino, Andrea Belotti
Belotti alifunga magoli 26 katika Serie A msimu uliopita na anatajwa kuwa kati ya washambuliaji hatari kwa sasa na watakaosumbu mbeleni. Kiasi cha pesa kinachohitajika kuvunja mkataba wake na klabu hiyo ni karibuni paundi milioni 89.

Chelsea wanatafuta mshambuliaji baada ya kumuuza Diego Costa na kumkosa  Fernando Llorente dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Belotti amekuwa akihusishwa na kuhamia Stamford Bridge.

Antonio Conte atakuwa anamfahamu vizuri nahodha huyo wa Torino kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye Serie A, na aliiambia bodi ya klabu ya Chelsea ijaribu kumsajili mshambuliaji huyo kabla haijaelekeza nguvu yao kwa Alvaro Morata mwezi Julai.

Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic
Kwa upande mwingine Manchester United wanaye Zlatan Ibrahimovic, ambaye anategemewa kurejea akitokea majeruhi kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji ambayo imeonekana kudorora kufuatia Romelu Lukaku kushindwa kuifungia timu yake katika michezo kadhaa iliyopita, lakini watahitaji kutafuta mbadala wa kudumu atakayechukua nafasi ya raia huyo wa sweeden mwenye miaka 36 pindi atakapomaliza mkataba wake.
Chelsea, Manchester United kuwania saini ya straika mwenye thamani ya paundi milioni 89 Chelsea, Manchester United kuwania saini ya straika mwenye thamani ya paundi milioni 89 Reviewed by Zero Degree on 11/16/2017 08:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.