Loading...

Eden Hazard aipa Real Madrid sharti moja


Ni dhahiri kwamba Eden Hazard ameiambia klabu ya Real Madrid atasaini mkataba wao kwa sharti moja.

Imekuwa ni tabia kwa klabu ya Real Madrid kujaribu kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa na walio bora katika sayari hii, Hazard ni mmoja wa wachezaji wanaotegemewa kusaini mkataba na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, taarifa ya tovuti ya Don Balon ya nchini Spain inadai mshambuliaji wa Chelsea, Hazard ameiambia Real Madrid kwamba, atakubali kuijunga na klabu hiyo ikiwa atapewa dhamana ya kuwa mmoja wa wachezaji wanaopewa heshima kubwa ndani ya klabu.

Lakini, Real Madrid tayari wana mshambuliaji wao mwenye uwezo mkubwa anayepewa heshima ya kipeeke ndani ya klabu hiyo.

Kumekuwa na tetesi zinazodai Real Madrid pia wanaweza kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane kwenye kipindi cha majira ya joto mwakani.

Lakini taarifa ya Don Balon inadai Eden Hazard ndiye chaguo la pekee la Zinedine Zidane lililobaki.

Kwa upande mwingine jambo hilo bado linaonekana kuwa gumu na Real Madrid watatakiwa kutia juhudi kubwa sana kuweza kufanisha kumnasa nyota huyo wa klabu ya Chelsea.


Licha ya wingi wa washambuliaji katika klabu ya Real Madrid, Hazard anataka apewe uhakika kwamba atakuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Zidane.

Katika kikosi cha Chelsea, Hazard ndiye chaguo lao la kwanza, licha ya kuwepo kwa wachezaji wengine kama Alvaro Morata, Pedro na Willian.

Ikiwa Real Madrid watafanikiwa kumnasa Eden Hazard, basi inawezekana ikawa ndio mwisho wa Gareth Bale kuitumikia klabu hiyo ya Uhispania.
Eden Hazard aipa Real Madrid sharti moja Eden Hazard aipa Real Madrid sharti moja Reviewed by Zero Degree on 11/09/2017 08:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.