Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 9 Novemba, 2017

Gabriel Jesus
Manchester City wana mpango wa kumpa Gabriel Jesus mkataba mpya utakao mfanya aingize paundi 100,000 kwa wiki licha ya kwamba mshambuliaji huyo wa Brazili bado hajatimiza mwaka mmoja tangu asajiliwe na klabu hiyo.

Tottenham imeingia kwenye orodha ya klabu zinazowania saini ya mshambuliaji wa Hamburg, Jann-Flete Arp, ambaye amekuwa kinara wa magoli katika kikosi cha Ujerumani chini ya miaka 17.

Arthur Melo
Manchester United wanampango wa kumsajili kiungo mwenye ubunifu mkubwa wa klabu ya Gremio, Arthur Melo. (Daily Mail)

Arsenal watahitaji kiasi cha kiasi cha paundi milioni 30 kwa ajili ya Mesut Ozil mwezi Januari ikiwa Manchester United bado wanamatammanio ya kumsajili Mjerumani huyo.

Christian Benteke ana matumaini ya kurejea katika kikosi cha Crystal Palace kitakapocheza dhidi ya Everton Jumamosi ya wiki ijayo. (Star)

Sergio Aguero anatazamia kuondoka Manchester City na kurejea kwenye klabu yake aliyochezea udogoni, Independiente ya nchini Argentina.

Ross Barkley
Chelsea wana mpango wa kutumia kiasi kikubwa cha fedha mwezi Januari kumnasa mshambuliaji mwenye jina kubwa na kuangalia uwezekano wa kumsajili Ross Barkley wa klabu ya Everton pia.

Jack Wilshere ana hofu kwamba, itampasa aihame klabu ya Arsena mwezi Januari kama atahitaji kushiriki kombe la dunia mwakani.

David Unsworth
David Unsworth amerejea mstari wa mbele kwenye kinyangianyiro cha kuwania kuziba pengo la Ronald Koeman Everton kwa sababu kuna mpasuko kati ya vigogo wa klabu hiyo juu ya utata wa nani anayefaa kuchukua nafasi hiyo.

Huddersfield wako tayari kutoa dau la paundi milioni 4 kumnasa beki wa klabu ya Barnsley, Andy Yiadom mwezi Januari(Mirror)

Alvaro Morata
Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata anataka kufikia rekodi ya kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kwa kushinda mataji ya Ligi Kuu Uingereza, Uhspania na Italia. (Express)

Wakurugenzi wa klabu ya Manchester United wanahofia Jose Mourinho yuko kwenye mikakati ya kuhamia Paris Saint-Germain.

Alvaro Morata hajutii uamuzi wake wa kujiunga na Chelsea na ana matumaini ya kusalia klabuni hapo kwa muda mrefu ujao.

Nahodha Lyon, Nabil Fekir ameziweka klabu za Ligi Kuu ya Uingereza kwenye mstari wa mbele kumsajili, baada ya kuvutiwa na Ligi hiyo maarufu duniani.

Viongozi wa klabu ya Everton watafanya mazungumzo na meneja wao wa muda, David Unsworth kuona kama anaweza kusalia hapo kwa muda mrefu zaidi.

Bayern Munich wako tayari kuachana na Robert Lewandowski na kumsajili Mauro Icardi kuziba pengo lake. (Sun)

Mipango ya usajili katika klabu ya Chelsea hatabadilishwa kufuatia mkurugenzi wao, Michael Emenalo kujiuzulu kwa kushtukiza wiki hii.

Sadio Mane
Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane amejiunga na kikosi cha Senegal akiwa pamoja na mtaalamu wa afya wa klabu hiyo kuhakikisha hapati madhara yoyote kutokana na majeraha aliyokuwa nayo katika paja lake. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 9 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 9 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/09/2017 12:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.