Loading...

Ibrahim Class amchakaza bondia kutoka Afrika Kusini


Mwanamasumbwi Ibrahim Class amewapa raha watanzania jana Jijini Dar es Salaam baada ya kumpiga Bondia Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini katika mchezo wa ndondi wa kimataifa baina yao uliokuwa na mizunguko kumi na mbili.

Katika pambano hilo lililohudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Ibrahim Class alishinda katika mzunguko wa kumi na mbili ambapo ameandika historia ya muda mrefu hapa nchini kwa mabondia kutofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema amefurahiswa sana na ushindi aliopata Ibrahim Class na kuahidi kumpa ushirirkiano zaidi ili aendelee kufanya vizuri katika mashindano mengine

“Siri ya mafanikio katika Michezo ni kufanya mazoezi,kujiamini kusikiiza mafundisho ya mwalimu pamoja na nidhamu,Ibrahim Class ni mwanamasumbwi anaepaswa kuigwa na mabondia na wanamichezo wengine wote kutokana na uwezo wake wa kujituma hivyo wanamichezo wanapaswa kuiga kutoka kwake ili wafanikiwe na kuitangaza nchi yetu kimichezo.” alisema Dkt. Mwakyembe.

Naye bondia Ibrahim Class ameishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyompa wakati wa mazoezi mpaka leo amefanikiwa kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania na ameahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi kila atakapokuwa ulingoni na kushinda mataji na mikanda mingi zaidi.
Ibrahim Class amchakaza bondia kutoka Afrika Kusini Ibrahim Class amchakaza bondia kutoka Afrika Kusini Reviewed by Zero Degree on 11/26/2017 05:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.