Loading...

Yanga yathibitisha kufanya usajili wa beki kutoka DRC


Klabu ya Yanga, imetangaza kumsainisha beki wa kati, Mkongo Fiston 'Festo' Kayembe Kanku ambaye alikuwa kwenye majaribio katika timu hiyo kwa muda mrefu.

Usajili huo wa mkataba wa miaka miwili umefikiwa kutokana na safu ya ulinzi kuonekana kutokuwa imara.

Kutua kwa Mkongo huyo kunamaanisha kuwa Mtogo, Vincent Bossou ambaye alikuwa njiani kurejea klabuni hapo kutofikiriwa.

Kupitia ukurasa wao wa Instragram, Yanga wameandika ujumbe huu: “Fiston 'Festo' Kayembe Kanku amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na #mabingwamara27 @yangasc akitokea Balende Fc ya DR CONGO.

“Festo anayeimudu vyema nafasi ya mlinzi wa kati amefanikiwa kusaini kandarasi hiyo baada ya majuma kadhaa ya majaribio chini ya kocha George Lwandamina.”

Usajili wa Kayembe unakuja muda mfupi baada ya Yanga jana kuruhusu goli la tano kwenye ligi kuu msimu huu ambalo lilipelekea timu hiyo kulazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons kunako dimba la uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Yanga yathibitisha kufanya usajili wa beki kutoka DRC Yanga yathibitisha kufanya usajili wa beki kutoka DRC Reviewed by Zero Degree on 11/26/2017 05:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.