Loading...

Chadema yajitoa kwenye uchaguzi wa madiwani katika kata tano mkoani Arusha

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuondoa Wagombea wake wa udiwani katika kata tano wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya Mawakala na Wagombea kutekwa na kushambuliwa kwenye vituo vya kupigia kura.

“Tumeagiza wagombea, mawakala na viongozi wetu wote wajitoe kwenye mchakato wa kata 5 za Arumeru Mashariki Kuna utekajinyara, mashambulizi, ubabe na ushenzi Wananchi wanaonewa sana Wagombea na viongozi wanatekwa, mawakala wanaondolewa vituoni, kura zinapigwa pasipokuwepo mawakala.”
Chadema yajitoa kwenye uchaguzi wa madiwani katika kata tano mkoani Arusha Chadema yajitoa kwenye uchaguzi wa madiwani katika kata tano mkoani Arusha Reviewed by Zero Degree on 11/26/2017 05:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.