Loading...

Italia yashindwa kufuzu fainali za kombe la dunia 2018


Mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia, wameshindwa kufuzu fainali za mwa 2018 nchini Urusi ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Sweden.

Hii ina maana kwamba Italia watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya kwanza ilikua mwaka 1930.

Kiungo Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro.


Wengi walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia sambamba na kucheza nyumbani.

Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa upande wao.

Nusura mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao lakini juhudi za mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake.

Matokeo haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.
Italia yashindwa kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 Italia yashindwa kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 Reviewed by Zero Degree on 11/14/2017 06:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.