Loading...

Korea Kaskazini yarusha Kombora lenye uwezo wa kuishambulia Marekani


Korea Kaskazini imefanikiwa kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lenye uwezo wa kufika eneo lolote la Marekani, hatua iliyopelekea Taifa hilo kufikia azimio lake la kuwa lenye nguvu za kinyuklia duniani.


Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Kitengo cha Habari cha Korea Kaskazini (KCNA), ilisema kombora hilo lenye uwezo mkubwa linalofahamika kwa jina la Hwasong-15, lilirushwa mapema siku ya Jumatano ambapo liliruka katika kimo cha kilomita 4,475 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 950 ndani ya dakika 53.

KCNA imesema kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un alishuhudia kufyatuliwa kwa kombora hilo na kutangaza kwamba, Taifa hilo sasa limekamilisha lengo lake la miaka mingi la kuwa Taifa lenye nguvu za kinyuklia.

Ripoti hiyo ya KCNA imeongeza kuwa, Korea Kaskazini kama Taifa lenye nguvu za kinyuklia na linalopenda amani, litafanya kila iwezalo kutekeleza lengo lake la kuleta amani na udhabiti duniani. Pia imesema silaha zake za ulinzi dhidi ya sera ya kibepari ya Marekani, hazitatishia kwenye Taifa lolote duniani iwapo maslahi ya Korea Kaskazini hayatakiukwa.
Korea Kaskazini yarusha Kombora lenye uwezo wa kuishambulia Marekani Korea Kaskazini yarusha Kombora lenye uwezo wa kuishambulia Marekani Reviewed by Zero Degree on 11/29/2017 12:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.