Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 29 Novemba, 2017

Beki wa Timu ya Taifa ya Brazil na Chelsea, David Luiz
Klabu ya Real Madrid iko tayari kujaribu kumnasa beki wa Chelsea, David Luiz mwezi Januari.

Jose Mourinho amewake kwenye mipango yake wachezaji wapya wenye uwezo mkubwa wa kutumia miguu yao ya kushoto akiweo Gareth Bale, Mesut Ozil, Antoine Griezmann, na Danny Rose.

AC Milan walikutana na wawakili wa Antonio Conte kujadili uwezekano wa kocha huyo kutua kuinoa klabu hiyo katika majira ya joto mwakani.

Sam Allardyce atateuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Everton ndani ya masaa 48 yajayo na anaamtaka Sammy Lee kama msaidizi wake.

Rio Ferdinand anaamini kwamba Zlatan Ibrahimovic ndio chanzo cha matatizo katika ufungaji kwa Romelu Lukaku.

Divock Origi
Divock Origi anafurahia maisha katika klabu ya Wolfsburg na anakiri kwamba maisha yake yajayo katika soka yanaweza kuwa mazuri zaidi akiwa nje ya klabu ya Liverpool. (Daily Mail)

Manchester City wako tayari kumpa David Silva mkataba mpya licha ya kwamba klabu nyingi za Italia na Uhispania zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Everton wanahofia kushindwa kumshawishi Sam Allardyce awe meneja wao mpya kufuatia mazungumzo yao na kocha huyo kuwa magumu.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anasistiza kwamba suala la usajili ndani ya klabu hiyo liko chini yake.

Petr Cech
kwa mujibu wa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, Petr Cech ana uwezo wa kucheza zaidi ya miaka mingine mitano.

Liverpool wanakumbana na ushindani mkubwa kutoka klabu ya Leicester katika kuwania saini ya nyota wa West Brom, Ahmed Hegazi kwa mkopo.

Arsenal ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Uingereza wanaotaka kumsajili nyota wa klabu ya Novara, Alessio da Cruz.

Nabil Fekir (lyon) anakaribia kujiunga na Arsenal, klabu hiyo ikiwa kwenye mipango ya kumtafuta mrithi wa Alexis Sanchez. (Mirror)

Nyota wa klabu ya Manchester City, Leroy Sane anatarajiwa kupewa ofa ya mkataba mpya kama zawadi kwa kiwango alichoonyesha msimu huu.

Sam Allardyce
Sam Allardyce atalipwa mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki kama meneja mpya wa klabu ya Everton.

Crystal Palace wanatazamia kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Bournemouth, Benik Afobe kwa paundi milioni 15 katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Klabu ya Watford inasistiza kwamba Richarlison hatauzwa mwezi Januari baada ya klabu nyingi kuonyesha nia ya kutaka kumsajili Mbrazil huyo. (Sun)

Meneja wa muda wa klabu ya Everton, David Unsworth amemuonya Sam Allardyce kwamba kuibadilisha klabu kwa haraka haitakuwa rahisi.

Eddie Howe ameahirisha kufanya tafrija ya kutimiza miaka 40 kuipa ushindi Bournemouth dhidi ya Burnley.

Meneja wa West Ham, David Moyes aeleza kwamba anaweza kustaafu kazi yake ya ukocha akiwa na klabu hiyo.

Mshambuliaji wa Watford, Richarlison
Chelsea na Spurs zametakiwa kutojaribu kumsajili nyota wa klabu ya Watford, Richarlison mwezi Januari. (Star)

Shakhtar Donetsk waliizuia klabu ya Everton kukutana na meneja wao, Paulo Fonseca. (Independent)

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amesema kwamba mpango wowote wa yeye kujiunga na Arsenal hautawezekana kwamwe. 

Chelsea wanatarajiwa kumsajili beki wa klabu ya Juventus, Alex Sandro mwezi Januari baada ya kushindwa kumsajili nyota huyo mwaka uliopita.
 (Express)

Andre Villas-Boas
Andre Villas-Boas amejiuzulu kazi ya ukocha katika klabu ya Shanghai SIPG na sasa anafikiria kupumzika kazi ya ukocha kwa muda. (Telegraph)

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte anadai kwamba hajaelezwa iwapo atalazimika kufanya usajili wa mchezaji yeyote katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 29 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 29 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/29/2017 03:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.