Loading...

TCRA yatoa onyo kwa wenye tabia ya kuwasajilia watu wengine laini za simu


Afisa wa masuala ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka Mamlaka ya mawasiliano tanzania TCRA, Bwana Walter Mariki amewataka watumiaji wa simu za mkononi kuacha tabia ya kuwasajilia watu wengine laini za simu ili kuepuka kuhusishwa na makosa ya kimtandao.

Bwana Mariki ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Katavi na kusema kuwa ni muhimu kwa watumiaji wa simu za mikononi kutoa taarifa sahihi wakati wa usajili.

Aidha kufuatia kuwepo kwa wimbi la tabia hatarishi katika mitandao mbalimbali ya kijamii Naibu Mkurugenzi wa TCRA masuala ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano bwana Thadayo Ringo amesisitiza wazazi kufuatilia kwa karibu matumizi ya mitandao kwa watoto.

Credits: ITV
TCRA yatoa onyo kwa wenye tabia ya kuwasajilia watu wengine laini za simu TCRA yatoa onyo kwa wenye tabia ya kuwasajilia watu wengine laini za simu Reviewed by Zero Degree on 11/29/2017 03:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.