Loading...

Lampard kurejea Chelsea?

Kiungo wa zamani wa klabu ya Chelsea, Frank Lampard
Frank Lampard anatajwa kuwa mstari wa mbele kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na mkurugenzi wa benchi la ufundi, Michael Emenalo katika klabu ya Chelsea.

Michael Emenalo
Emenalo alijiuzulu wadhifa huo mwanzoni mwa wiki hii baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka 6, ikiwa ni kinyume na mapenzi ya mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich, ambaye hakuwa na mpango wowote wa kufanya mabadiliko katika nafasi hiyo.

Chelsea sasa wameanza mchakato wa kumtafuta mtu atakayeziba pengo hilo na kwa mujibu wa 'The Express', Lampard ni miongoni mwa wanaotarajiwa kupewa kibarua hicho.

Kwa sasa, Marina Granovskaia ndiye anayetekeleza majukumu hayo kwa muda ambao Chelsea wakiwa katika harakati za kumtafuta mtu sahihi wa kuchukua nafasi hiyo.

Andrea Pirlo
Nyota wa timu ya Taifa ya Italia, Andrea Pirlo pia ametajwa miongoni mwa wanaoweza kupewa nafasi hiyo, ikiwa tayari ametangaza kustaafu mchezo kucheza soka mwanzoni mwa wiki hii.
Lampard kurejea Chelsea? Lampard kurejea Chelsea? Reviewed by Zero Degree on 11/08/2017 06:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.