Loading...

Mbeya City kupeleka barua TFF kupinga bao la Kichuya

Shiza Kichuya
Uongozi wa klabu ya Mbeya City umesema kuwa una mpango wa kupeleka barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga bao walilofungwa kwenye mchezo uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Champion, Mbeya City wanataka kupata vipimo au uhakika wa bao hilo kama kweli lilikuwa sahihi au la kwa kuwa wanaamini mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga.

Mchezo huo uliochezwa Jumapili, ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mbeya City, bao lilofungwa na Shiza Kichuya lakini klabu hiyo imesema kuwa bao hilo siyo halali kwa kuwa mfungaji alikuwa ameotea.

Taarifa ya hiyo inasema kwamba, Katibu wa Mbeya City, Emanuel Kimbe amesema kuwa, kwa sasa wanatafakari cha kufanya na baada ya hapo watapeleka malalamiko yao TFF.

“Kila mtu ameona, tafsiri ya offside ni kuingilia mchezo, Kichuya alikuwa offside kabla ya mpira haujamfikia na mpira ulimkuta yeye na kuanza kuukokota na kufanikiwa kufunga.

“Mwamuzi aliyechezesha mechi yetu ndiye aliyechezesha fainali ya FA kati ya Simba na Mbao kule Dodoma na maamuzi yake yalikuwa ya utatautata hivyohivyo na alilalamikiwa, inatupa mashaka na kujiuliza kwa nini inakuwa hivi, lakini tutaangalia na kufanya maamuzi ndani ya saa 72 kuamua kitu cha kufanya kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi lakini kulalamika TFF.

“Ligi imekuwa ngumu na yenye ushindani wa hali ya juu lakini tunapata changamoto ya kimaamuzi kwenye ligi hivyo tunajikuta tunashindwa kufanya vizuri katika baadhi ya mechi,” alisema Kimbe.
Mbeya City kupeleka barua TFF kupinga bao la Kichuya Mbeya City kupeleka barua TFF kupinga bao la Kichuya Reviewed by Zero Degree on 11/08/2017 12:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.