Loading...

Bomu laua wanafunzi watatu mkoani Kagera

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustino Olomi
Mlipuko unaosadikiwa kuwa ni bomu umeuwa wanafunzi watatu wilayani Ngara mkoani Kagera na kujeruhi wengine kadhaa katika shule ya msingi Kihinga wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba wanafunzi hao walikuwa wakati wa mapumziko ya saa nne, na ndipo mlipouko huo ulipotokea na kusababisha madhara hayo.

Jeshi la polisi tayari lipo eneo la tukio kufuatilia na kufanya uchunguzi, na taarifa kamili zitatolewa baada ya muda mfupi.
Bomu laua wanafunzi watatu mkoani Kagera Bomu laua wanafunzi watatu mkoani Kagera Reviewed by Zero Degree on 11/08/2017 12:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.