Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 8 Novemba, 2017


Kufuatia kitendo cha David Luiz kuachwa nje ya kikosi kilichoivaa Manchester United, mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich anafanya uchunguzi wa kina kujua kama kuna tatizo kubwa kati ya meneja Antonio Conte na wachezaji.

Newcastle wako tayari kufanya mpango wa kumnasa mshambuliaji wa Liverpool, Danny Ings kwa mkopo mwezi Januari.

Angel Di Maria na Lucas Moura
PSG matumaini ya kumuuza Angel Di Maria na Lucas Moura mwezi Januari, baada ya UEFA kuwaambia kwamba wanapashwa kuzalisha kiasi cha paundi milioni 70 kama wanataka kukidhi vigezo vya haki za kimchezo.


Luke Shaw anatarajia kuipotezea ofa ya kujiunga na Fenerbahce mwezi Januari na kubakia Old Trafford apiganie nafasi yake kikosini. (Daily Mail)

Real Madrid wanafanya mpango wa usajili wa kushitukiza wa nyota wa Man United, Juan Mata ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu.

Lionel Messi amewachagulia Barcelona majina matatu ikiwa watashindwa kumsajili Philippe Coutinho kutokea Liverpool, la kwanza ni Thomas Lemar wa Monaco, pili ni, Nabil Fekir wa Lyon na tatu ni Riyad Mahrez wa Leicester City.

Joe Gomez (Liverpool), anataka kujihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Uingereza kwenye Kombe la Dunia baada ya kuitwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Ujerumani na Brazil. (Express)

Ili kusaini mkataba mpya, Mesut Ozil anataka apewe jezi namba 10 Arsenal ambayo kwa sasa inavaliwa na Jack Wilshere.

Mmoja wa wamili wa klabu ya West Ham, David Sullivan anasema kwamba, uteuzi wa David Moyes ni kama mchezo wa bahati nasibu na hawana chaguo jingine la kuitwaa nafasi yake itakapofika mwisho wa msimu. (Sun)

Slaven Bilic aliwaita wachezaji wake baada ya kufukuzwa kazi siku ya Jumatatu kuwauliza ni wapi wanahisi alikosea, na wengi wao wakamlalamikia ni kwanini aliruhusu hatua hizo kuchukuliwa.


Paul Pogba akiwa mazoezini
Paul Pogba anategemewa kurejea kutokea majeruhi katika mechi ya Manchester United dhidi ya Newcastle baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Southampton wanamvizia aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City, Stevan Jovetic awasaidi kumaliza matatizo yao katika suala zima la ufungaji chini ya meneja, Mauricio Pellegrino. (Mirror)

Uwezekano wa Sam Allardyce kutwaa kazi ya umeneja wa klabu ya Everton unazidi kuwa mgumu kwa sababu ya makubaliano juu ya mkataba kushindwa kufikiwa, ikiwa yeye anataka mkataba mrefu na wakati klabu hiyo inatazamia kumpa kibarua hicho kwa muda uliosalia hadi kumalizika kwa msimu huu.

Winga wa Southampton, Nathan Redmond amesema kuwa hali ya wachezaji wenzake kimchezo haijaathiriwa na sakata la usajili wa Virgil van Dijk lililotikisa kipindi cha majira ya joto.

Nyota wa Crystal Palace, Cenk Tosun anasema kwamba hana mapango wa kuhamia Uingereza kwani anafurahia maisha aikiwa na Besiktas. (Star)

David Luiz anatazamia kurejea kufanya mazoezi na Chelsea siku ya Jumatano baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza dhidi ya Manchester United.

Chelsea wanapitia upya mfumo wao wa utawala baada ya kujiuzulu kwa mkurugenzi wa ufundi, Michael Emenalo. (Guardian)

Adam Lallana
Adam Lallana atacheza kwenye mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu ya Liverpool wiki ijayo akitokea majeruhi. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 8 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 8 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/08/2017 11:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.