Loading...

Messi ataja klabu ya EPL anayoiogopa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi
Nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesema kwamba vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City ni moja kati ya klabu mbili zenye uwezo mkubwa zaidi kwenye michuano ya Klabu Bingwa.

Ligi ya Mabingwa msimu huu inaerekea mwishoni katika hatua ya makundi, ikiwa umebaki mzunguko mmoja pekee.

Klabu ya Barcelona tayari imejikatia tiketi ya kushiriki hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambayo droo yake itaanza tarehe 11 ya mwezi desemba na raia huyo wa Argentina amekuwa akifanya uchunguzi wa kikwazo kikubwa kwa matumaini ya Barcelona kushinda taji la tano la Ligi ya Mabingwa.

“Manchester City ni moja kati ya timu bora kwa sasa, pamoja na PSG,” alisema Lionel Messi wakati akizungumza na Gazeti la Marca la Uhispania.

“Kumekuwa na timu mbili ambazo ni bora zaidi hadi hivi sasa, lakini msimu bado ni mrefu sana.”

Real Madrid watamaliza hatua ya makundi katika nafasi ya pili kwenye Kundi 'H' baada ya Tottenham kuwapiku na kuwa vinara wa kundi hilo, lakini Messi anatambua kwamba vijana hao wa Zinedine Zidane sio wa kubeza, ikiwa na wao pia wako kwenye harakati za kuwinda Taji la michuano hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

“Sijawatoa Real Madrid kamwe kwa uwezo walionao na uzoefu wao, hata kama hawapati matokeo ambayo watu wanayategemea. Bayern Munich, pia ni timu ambayo itapigana hadi mwisho wa msimu, lakini ni dhahiri kwamba, kwa sasa, Manchester City na PSG ni bora zaidi.”
Messi ataja klabu ya EPL anayoiogopa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya Messi ataja klabu ya EPL anayoiogopa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya Reviewed by Zero Degree on 11/27/2017 06:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.