Loading...

Msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] baada ya mechi za katikati ya wiki

Wachezaji wa Arsenal wakishangilia bao
Baada ya Jumanne ya Novemba 28, 2017 kuchezwa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2017/2018, jana Jumatano ya Novemba 29 ilichezwa michezo sita ya Ligi Kuu Uingereza, Arsenal walicheza dhidi ya Huddersfield, Chelsea dhidi ya Swansea, Manchester City dhidi ya Southampton, Bournemouth dhidi ya burnley, Everton dhidi ya West Ham na Liverpool dhidi ya Stoke City.

Michezo hiyo ilimalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Huddersfield, magoli yakifungwa na Lacazette dakika ya 3, Giroud dakika ya 68 na 87, Sanchez dakika ya 69 na Ozil dakika ya 72 na ushindi huo umeifanya Arsenal kuendelea kuwepo nafasi ya 4 katika msimamo wa EPL.

Wakati Man City wakiwa katika uwanja wao wa Etihad wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Southampton, goli la kwanza lilifungwa na mchezaji wao wa kibelgiji Kevin De Bruyne dakika ya 47 na la pili likifungwa katika dakika za nyongeza na Raheem Sterling huku goli la Southampton likifungwa na Romeu katika dakika ya 75.

Matokeo ya Mechi nyingine ni kama ifuatavyo:

Jumanne (Tar 28 Novemba, 2017):
  • Brighton 0-0 Crystal Palace
  • Leicester City 2-1 Tottenham
  • Watford 2-4 Manchester United
  • West Brom 2-2 Newcastle
Jumatano (Tar 29 Novemba, 2017):
  • Bournemouth 1-2 burnley
  • Chelsea 1-0 Swansea
  • Everton 4-0 West Ham
  • Stoke City 0-4 Liverpool
Msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza hadi hivi sasa:

Msimamo EPL

Msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] baada ya mechi za katikati ya wiki Msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] baada ya mechi za katikati ya wiki Reviewed by Zero Degree on 11/30/2017 10:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.