Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 30 Novemba, 2017

Mshanbuliaji wa Manchester United, Anthony Martial
Matamanio ya klabu ya Manchester United kuwasajili Antoine Griezmann na Gareth Bale yamepungua kufuatia kuimarika kwa kiwango cha mshambuliaji wao, Anthony Martial.

Florentino Perez amemuonya golikipa wa Manchester United, David De Gea kwamba asipokubali kusaini mkataba na Real Madrid katika majira ya joto mwakani wataelekeza nguvu zao kwa golikipa wa Chelsea, Thibaut Courtois.

Watford wana jaribu kufanya hesabu za kumsajili mchezaji wa Leicester, Islam Slimani kwa mkopo mwezi Januari.

Liverpool wana andaaa ofa ya paundi milioni 53 kwa ajili ya winga wa Sporting Lisbon, Gelson Martins.

Jakub Jankto
Arsenal wanatarajiwa kufanikisha usajili wa kiungo wa Czech, Jakub Jankto licha ya kwamba klabu za AC Milan na Juventus zimeshajitokeza kutaka kumsajili nyota huyo. (Mirror)

Zlatan Ibrahimovic anataka Manchester United imsajili nyota wa klabu Real Madrid, Gareth Bale.

Antoine Griezmann kwa mara nyingine ameifungulia milango klabu ya Manchester United.

Chelsea imeonekana kuwa msatri wa mbele kutaka kushitukiza usajili wa nyota wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil.

Emerson Palmieri
Klabu ya Liverpool inafanya mpango wa kumsajili beki wa Roma, Emerson Palmieri katika majira ya joto baada ya kupata uhakika wa ubora wa afya ya mchezaji huyo.

Meneja wa klabu ya Watford, Marco Silva amekiri kwamba nyota anayewindwa na klabu ya Chelsea na Tottenham, Richarlison anaweza kuondoka katika klabu hiyo. (Star)

Alan Pardew
Alan Pardew ametetea rekodi zake kama kocha kwenye Ligi Kuu ya Uingereza na kusema kwamba atarejesha heshima yake akiwa na klabu ya West Bromwich Albion.

Real Madrid wana matumaini ya kumnasa David Luiz ifikapo mwezi Januari kufuatia mgogoro ulioibuka kati ya beki huyo na meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte. (Telegraph)

Arsenal wanakaribia kumnasa kiungo wa klabu ya Udinese, Jakub Jankto.

Imeripotiwa kwamba, Laurent Koscielny ameiambia klabu yake ya zamani Lorient kuwa anataka kuondoka Arsenal na kurejea Ufaransa.

Alex Sandro
Chelsea inatarajiwa kurejesha mapenzi yake kwa Alex Sandro kama David Luiz atajiunga na klabu ya Real Madrid.

Aliyekuwa kiungo wa AC Milan na Real Madrid, Kaka amesema kwamba hakujiunga na klabu ya Manchester City mwaka 2009 kwa sababu alihofia harakati za kuimarisha kikosi walizokuwa nazo Waingereza hao.

Kiungo wa Real Madrid, Luka Modric anatuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha paundi 770,000 kati ya mwaka 2013 na 2014. (Sun)

Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Gareth Southgate
Meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Gareth Southgate atazialika familia za wachezaji wake kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi katika majira ya joto yajayo.

Daley Blind anahofia kuuzwa na klabu yake ya Manchester United katika majira ya joto mwakani. (Times)

Keylor Navas amemuweka Rais wa Real Madrid, Florentino Perez katika wakati mgumu kufuati kugoma kuondoka na kusababisha uwezekano wa klabu hiyo kumsajili Kepa kuwa mgumu. 

Lionel Messia aitibulia Real Madrid mipango ya kumsajili raia mwenzake wa Argentina anayekipiga katika klabu ya Inter Milan, Mauro Icardi. 

Florentino Perez ana mpango wa kuwaunganisha Eden Hazard na Neymar katika klabu ya Real Madrid. (Don Balon)

Alan Pardew ana imani kwamba klabu yake ya West Brom itakuwa na mwazo mzuri chini yake kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Crystal Palace. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 30 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 30 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/30/2017 05:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.