Loading...

Ndikumana azikwa nchini Rwanda, mamia wajitokeza kumzika


Mwili wa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Hamadi Ndikumana Katauti na mume wa muigizaji wa filamu Bongo, Irene Uwoya, umezikwa jana katika makaburi yaliyopo kwenye mji wa Nyamirambo nchini Rwanda.

Baba mzazi wa Ndikumana
Ndikumana ambaye pia ni baba wa watoto wawili huku mmoja akiwa amezaa na Irene Uwoya, amezikwa na mamia ya wadau wa soka nchini humo wakiwemo mashabiki wa klabu ya Rayon Sport, ambayo alikuwa akifanyia kazi kama kocha msaidizi.

Taarifa zaidi zinadai kwamba Irene Uwoya hakuhudhuria mazishi hayo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Ndikumana alifariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake nchini Rwanda, na kuacha majonzi makubwa kwa wapenzi wa soka na watu wake wa karibu, kutokana na kifo chake kilichotokea ghafla bila kuumwa.

Mamia wakusanyika kumzika Ndikumana
Ndikumana azikwa nchini Rwanda, mamia wajitokeza kumzika Ndikumana azikwa nchini Rwanda, mamia wajitokeza kumzika Reviewed by Zero Degree on 11/16/2017 04:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.