Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 16 Novemba, 2017

Kurt Zouma
Ryan Shawcross (Stoke City) anashangaa ni kwanini Chelsea walimruhusu Kurt Zouma aondoke kwa mkopo, kwani anadai ni mmoja kati ya mabeki hatari sana katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Sunderland watahamishia majeshi yao kwa meneja wa Ireland, Michael O'Neill kama meneja wa Barnsley, Paul Heckingbottom atakataa ofa yao.

Chris Smalling, Jack Wilshere, Daniel Sturridge, Danny Welbeck na Theo Walcott hawako kwenye mipango ya Gareth Southgate kwenye kombe la dunia 2018.



Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wanakazania kupata nafasi ya kushiriki mechi ya Manchester United dhidi ya Newcastle wikendi hii.

Real Betis wanaamini watafanikiwa kumsajili kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere kama mchezaji huru katika majira ya joto mwakani.

Sven Mislintat
Arsenal wanamfukuzia mkurugenzi wa ufundi wa Borussia Dortmund, Sven Mislintat kuchua nafasi ya Steve Rowley. (Sun)

Jose Mourinho anasema ataleta wachezaji wenye umri mdogo  Manchester United na Scott McTominay ndiye anayefuata kwenye orodha ya wachezaji anaowahitaji.

Kwa sasa klabu ya Liverpool inashindana na Arsenal kwa kuwa na tiketi za gharama kubwa zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

David Unsworth
Everton wanalazimika kubakia na David Unsworth baada ya Sam Allardyce na Marco Silva kukataa kukinoa kikosi chao. (Mirror)

Klabu ya West Brom inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza inakaribia kumfukuza kazi meneja, Tony Pulis.

John O'Shea, Glenn Whelan, Jon Walters, Wes Hoolahan na Daryl Murphy wanatarajiwa katangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya Jamhuri ya Ireland kushindwa kukata tiketi ya kushiriki kombe la dunia. (Star)

Pep Guardiola yuko tayari kuongeza mkataba wake na klabu ya Manchester City mbele zaidi ya mwaka 2019.

Mshambuliaji wa Tottenham, Dele Alli 
Familia ya Dele Alli imefanya mazungumzo na Jorge Mendes kuhusu kumuuza nyota huyo wa klabu ya Tottenham kwa kampuni ya uwakala wa wachezaji ya Gestifute mwakani. (Daily Mail)

Sergio Aguero yuko tayari kujiunga na kikosi cha Manchester City kitakachoivaa Leicester Jumamosi siku chache tu baada ya kuzua hufo kwa kuanguka uwanjani akiwa na Argentina. (Express)

Everton wameshindwa kumnasa meneja wa Watford, Marco Silva kwa paundi milioni 10. (Telegraph)


Henning Berg
Aliyekuwa beki wa klabu ya Rangers zamani, Henning Berg ameomba kazi ya umeneja katika klabu hiyo. (Daily Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 16 Novemba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 16 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/16/2017 06:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.