Loading...

Papa Francis azungumzia suala la kushikwa na usingizi wakati wa maombi

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amekiri kwamba mara nyengine yeye hushikwa na usingizi wakati anapoomba
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amekiri kwamba mara nyengine yeye hushikwa na usingizi wakati anapoomba.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amekiri kwamba mara nyengine yeye hushikwa na usingizi wakati anapoomba
''Wakati ninapoomba , mara nyengine mimi hushikwa na usingizi'', alisema katika kipindi kimoja cha kanisa hilo cha TV2000 kilichochapishwa katika mtandao wa You tube.

''Mtakatifu Theresa pia alikuwa akilala'', alisema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 kuhusu mtakatifu huyo wa karne ya 19.

Lakini akasema kuwa kushikwa na usingizi wakati wa maombi huwa ''kunamfurahisha mungu na kwamba Wakristo walitakiwa kuhisi kama watoto wanaolalia mkono wa baba yao''.


Ripoti zinasema kuwa papa Francis hulala mwendo wa saa tatu na kuamka saa kumi alfajiri kila asubuhi.

Raia huyo wa Argentina amekuwa kiongozi wa kanisa katoliki tangu 2013 na amekuwa na ratiba iliyo na mambo mengi ya ziara za kigeni na mikutano ya kuonekana hadharani.

Amekuwa maarufu kwa baadhi ya mabadiliko na uwazi katika uongozi wake hususan katika utumizi wa lugha ya moja kwa moja inayoeleweka.
Papa Francis azungumzia suala la kushikwa na usingizi wakati wa maombi Papa Francis azungumzia suala la kushikwa na usingizi wakati wa maombi Reviewed by Zero Degree on 11/01/2017 07:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.