Loading...

Wachina wakamatwa wakitorosha mchanga wa madini


Jeshi la polisi mkoa wa Mara limewakamata raia watano wa nchi ya china wanaomiliki mgodi wa madini wa Zem Tanzania Limited katika kijiji cha Nyasirori wilayani Butiama, wakitorosha mchanga wenye madini mbalimbali maarufu kama makinikia kwenda jijini Dar –es- salaam kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Japhary Mohamed, amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara lilipata taarifa kuhusu wawekezaji hao kuandaa mpango wa kutorosha mchanga huo wa madini, na hivyo Jeshi la Polisi lilizalimika kuweka mtego ambao umewezesha kukamatwa kwa magari mawili katika barabara kuu ya Mwanza-Musoma yakiwa na masanduku 14 yenye mchanga huo wenye madini ya aina mbalimbali.

Kwa sababu hiyo Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi mkoani Mara,ametoa onyo kali kwa wawekezaji ambao wamezoea kufanya biashara za ujanjaujanja kwa kutorosha rasilimali za nchi na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika.

Source: ITV
Wachina wakamatwa wakitorosha mchanga wa madini Wachina wakamatwa wakitorosha mchanga wa madini Reviewed by Zero Degree on 11/01/2017 06:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.