Siri imefichuka, ...kwanini Ronaldo aligoma kubadilishana jezi na mchezaji wa Girona
Real Madrid walifungwa goli 2-1 na timu iliyopanda daraja msimu huu. Magoli yalifungwa na Cristian Stuani na Cristian Portu kwa upande wa Girona wakati goli la Madrid likifungwa na Isco.
Kwa kichapo hicho, vijana wa Zinedine Zidane sasa wanakuwa nyuma ya vinara wa La Liga, FC Barcelona kwa pointi nane, ikiwa tayari mechi 10 zilishachezwa.
Baada ya mechi hiyo kumalizika, nahodha msaidizi wa Girona, Granell alijaribu kumuomba Cristiano Ronaldo wabadilishane jezi, lakini mshambuliaji huyo wa Real Madrid alikataa na kujikuta akiwashangaza mashabiki wengi.
Kwa mujibu wa taarifa ya 'Fricandó Matiner' iliyotafsiriwa na mtandao wa Sport, Granell amefichua kwanini Ronaldo hakutaka kubadilishana naye jezi na jibu alilotoa kufuatia ombi hilo.

"Aliniambia kwamba, hataki kufanya hivyo kutokana na jinsi tulivyo tawala mchezo katika dakika za mwisho," alisema Granell.
"Aliniambia nilionesha kiwango kizuri, lakini hakuwa tayari kubadilishana jezi na mimi.
"Nilimuambia (Ronaldo) kwamba, matokeo tuliyoyapata hayakutokana na miujiza, lakini ilitokana na uzoefu tuliopata miaka ya nyuma na juhudi ya kusaka ushindi."
Siri imefichuka, ...kwanini Ronaldo aligoma kubadilishana jezi na mchezaji wa Girona
Reviewed by Zero Degree
on
11/01/2017 04:55:00 PM
Rating: