Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 1 Novemba, 2017

Kiungo wa Manchester United, Michael Carrivk
Mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Michael Carrivk, 36 hana mpango wa kuondoka Old Trafird licha ya Leicester City, West Bromwich Albion na Aston Villa kuonyesha dalili za kutaka kumsaini.

Arsenal na Chelsea wote wanammzea mate aliyekuwa kipa wa Liverpool Peter Gulacsi, 27, kutoka RB Leipzig.(ESPN)

Thomas Lemar
Arsenal italazimika kushindana na klabu za Barcelona na Liverpool ikiwa watahitaji kumsajili winga wa Monaco, Thomas Lemar, ambaye ana umri wa miaka 21 hivi sasa. (Telegraph)

Sam Allardyce atafanya mazungumzo na Everton kuhusu nafasi iliyo wazi ya umeneja lakini anataka mkataba mzuri iki kuchukua nafasi hiyo. (Sun)

Mshambuliajia wa Swansea Tammy Abraham, 20 ambaye yuko Swansea kwa mkopo atakaa fursa ya kuichezea Nigeria na badala yake kuamua kusubiri kuichezea England. (Times )

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Roma Radja Nainggolan anasema kuwa hakufikiria kujiunga na Chelsea, ambao waihusishwa na kumsaini mchezaji huyo wa miaka 29. (Independent)

Mchezaji wa safu ya kati wa Monaco, Fabinho, 24, amefichua kuvunjika kwake moyo baada ya jitihada zake za kuhamia Manchester United na Paris St-Germain kugonga mwamba mwaka uliopita. (Sports Illustrated)

Claudio Ranieri
Leicester City hawakuwasiliana na meneja wa zamani Claudio Ranieri, ambaye sasa anaongoza klabu ya Ufaransa Nates, kuhusu kurejea kwake katika klabu hiyo kama meneja. (Leicester Mercury)

Manchestrer United ndio wanaweza kumsajili mlinzi wa Celtic Kieran Tierney, 20, na mshambuliaji wa umri wa miaka 21 Moussa Dembele. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 1 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 1 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/01/2017 01:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.