Loading...

TANZIA: Hamad Ndikumana afariki dunia ghafla


ALIYEKUWA mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, mchezaji Hamad Ndikumana (39) kutoka nchini Rwanda amefariki usiku wa kuamkia leo, chanzo cha kifo chake kikisemekana ni matatizo ya moyo ambapo jana alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida.


Kataut beki wa zamani wa Rayon Sports na mume wa muigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya amefariki dunia baada ya kuugua ghafla.

Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza Kataut alikuwa mazoezini jana asubuhi.

Wakati anapoteza maisha, Kataut alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.

Mara ya mwisho, Kataut aliichezea Stand United ya Shinyanga wakati akitokea Cyprus.

Alikuja nchini mara ya mwisho wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.
TANZIA: Hamad Ndikumana afariki dunia ghafla TANZIA: Hamad Ndikumana afariki dunia ghafla Reviewed by Zero Degree on 11/15/2017 11:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.