Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 15 Novemba, 2017

Neymar
Julian Draxler anasema kwamba Neymar anastahili kupewa marupurupu yote ambayo klabu ya Paris Saint-Germain inampa kwa sababu Mbrazil huyo ni 'supastaa'.

Italia wanataka kumrejesha Antonio Conte baada ya aibu waliyoipata kwa kushindwa kufuzu kombe la dunia 2018.

Arsenal wako tayari kuachana na mpango wa kumsajili nyota wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar.

Meneja wa West Ham, David Moyes anataka kumfanya beki wa Brighton, Lewis Dunk kuwa mchezaji wake wa kwanza atakayemsajili mwezi Januari.

Wolves wana matumaini ya kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa, kwa kumsajili nyota wa Fiorentina, Nicolai Jorgensen.

Meneja msaidizi wa Bristol City, Dean Holden ni mmoja wa wanaowania nafasi ya kuinoa Bury inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza. (Mirror)

Andrea Belotti
Chelsea wamepata pigo kubwa katika kujaribu kumsajili Andrea Belotti baada ya rais wa klabu yaTorino, Urbano Cairo kusema kuwa amefanya mawasiliano na rais wa Real Madrid, Florentino Perez kuhusiana na mshambuliaji huyo.

Manchester United wametumia zaidi ya paundi milioni 52 kulipa mishahara kwa wachezaji majeruhi tangu mwaka 2014.

Sadio Mane amekubali kuwa huwa anajawa na hofu kuitazama Liverpool ikicheza akiwa nje.

Thomas Vermaelen amekiri tena kuwa anajutia kubakia Barcelona msimu uliopita. (Sun)

Barcelona wanategemewa kufanya kikao na Liverpool mwezi huu kuhakikisha uhamisho wa Philippe Coutinho unafanikiwa mwezi Januari.

Chelsea wanatazamia kumuuza Willian mwezi January wapate pesa za kumsajili winga wa Paris Saint-Germain, Lucas Moura.

Winga wa Leicester, Ahmed Musa ana matumaini ya kuungana na Leonid Slutsky katika klabu ya Hull City wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa ifikapo mwezi Januari. (Express)

Watford wamekataa ofa ya pili ya paundi milioni 8 na nusu iliyotolewa na klabu ya Everton kwa ajili ya kumnasa Marco Silva awe mrithi wa Ronald Koeman.

Joe Gomez
Liverpool wanalazimika kuilipa Charlton paundi 250,000 baada ya Joe Gomez kushiriki mechi ya kimataifa akiwa na kikosi cha Uingereza dhidi ya Brazil.

Arsenal watarejesha mapenzi yao kwa Raheem Sterling mwezi Januari kama sehemu ya makubaliano yao na klabu ya Manchester City ili kumwachia Alexis Sanchez. (Daily Mail)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho kwa sasa anamtazama Carlos Soler anayeichezea klabu ya Valencia kama chaguo lake la kwanza la usajili mwezi Januari.

Everton wako tayari kuongeza mshahara wa Marco Silva na kumpa pesa za kutosha kufanya usajili mwezi Januari kujaribu kumshawishi meneja huyo wa Watford ahamie Goodison Park. (Independent)

Brendan Rodgers amemuweka mstari wa mbele beki wa Reading, Liam Moore kwenye orodha ya wachezaji anaowahitaji mwezi Januari.

Paul Lambert
Morten Wieghorst anasema kuwa Paul Lambert ndio mtu pekee wa kuingoza Scotland ifanikiwe kuondokana na hali yake ya sasa.

Aliyekuwa winga wa Manchester United, Chris Eagles anaweza kuwa wa kwanza kusajiliwa na Owen Coyle katika klabu ya Ross County endapo ataonyesha ubora kwenye majaribio. (Daily Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 15 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 15 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/15/2017 07:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.