Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 18 Novemba, 2017

Petr Cech
Peter Cech amekiri kuchanganyikiwa kwa kuona kwamba tayari klabu ya Arsenal imeondolewa kwenye mbio za kuwania Taji la Ligi Kuu ya Uingereza.

Manchester United wataanzisha mpango mwingine kujaribu kumsajili nyota wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale.

Roy Hodgson anaamini kwamba, Wayne Rooney alitakiwa kuwa bado anaichezea timu yake ya taifa ya Uingereza. (Mirror)

Marouane Fellaini
Klabu ya Galatasaray imeingia kwenye kinyang'anyiro kuwania saini ya nyota wa Manchester United, Marouane Fellaini.

Chris Coleman atalipwa paundi 750,000 kwa mwaka kama meneja wa klabu ya Sunderland baada ya kujiuzulu Wales.

Riyad Mahrez anasistiza kwamba ana furahia kuwa Leicester licha ya kwamba anataka kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Hulk
Nyota wa Timu ya Taifa ya Brazil, Hulk anadai ana nafasi ya kujiunga na Ligi Kuu ya Uingereza mwezi Januari. (Sun)

Tony Pulis ameiambia bodi ya klabu ya West Brom kufikiria kabla ya kuchukua uamuzi wa kumfukuza kazi.

Meneja wa klabu ya Crystal Palace, Roy Hodgson amewaonya wachezaji wake kuwa wanatakiwa kumdhibiti mshambuliaji wa klabu ya Everton, Wayne Rooney.

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amekataa kuzungumzia kuhusiana na uhamisho wa nyota wa klabu ya PSG, Neymar. (Star)

Bayern Munich wanakaribia kufikia makubaliano na klabu ya Hoffenheim kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo, Sandro Wagner.

Jurgen Klopp atampa Dominic Solanke nafasi ya kutosha uwanjani katika klabu ya Liverpool.

Arsene Wenger anasema hatachapisha kitabu kinachozungumzia historia ya maisha yake akiwa na klabu ya Arsenal.

Danny Drinkwater
Antonio Conte anasema kwamba, kwa kitendo cha meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Gareth Southgate kumwacha Danny Drinkwater ni sawa na kumpatia nafasi ya kufanya maamuzi. (Daily Mail)

Real Madrid wana matumaini kwamba, mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez atahamia Manchester City ili wapate wasaa wa kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo, Sergio Aguero. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 18 Novemba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 18 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/18/2017 05:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.