Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 26 Novemba, 2017

Zidane akiwa na Gareth Bale
Meneja wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amezungumzia umuhimu mkubwa wa uwepo wa Gareth Bale katika klabu hiyo, licha ya kwamba, nyota huyo anahusishwa na uhamisho kuelekea Manchester United. (Telegreph)

Martin O'Neill ni wa kwanza katika orodha ya makocha watatu wanaotarajiwa kupewa kazi ya ukocha katika klabu ya Everton.

Mshambuliaji wa klabu ya Crystal Palace, Christian Benteke ataachana na dili la kujiunga na Ligi Kuu ya China abakie kuisaidia klabu yake isishuke daraja.

Mesut Ozil anategemewa kuanza mazungumzo na klabu ya Barcelona, huku mkataba wake na Arsenal ukitarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu.

 Andy Robertson
Liverpool hatakubali kumwachia Andy Robertson kwa mkopo mwezi Januari, licha ya kwamba anahusishwa na kusaini mkataba na klabu ya Hull City msimu huu. (Sun)

Meneja wa klabu ya Newcastle, Rafa Benitez anamtaka beki wa Manchester United, Luke Shaw kwa mkopo.

Klabu ya Liverpool inatemewa kuingia vitani dhidi ya Arsenal kusaka saini ya nyota wa PSG, Julian Draxler, kutokana na nyota huyo kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza mbele ya Unai Emery.

PSG wako mbele ya Manchester City kwenye kinyang'anyiro cha kusaka saini ya mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez.

Real Madrid wanafanya mpango wa kumsajili nyota wa Manchester United, Anthony Martial kwa paundi milioni 80.

Bill Kenwright na Farhad Moshiri wanakaribia kupewa majukumu ya kukinoa kikosi cha Everton.

Adam Masina
Tottenham wanatazamia kumsajili nyota wa klabu ya Bologna, Adam Masina achukue nafasi ya Danny Rose licha ya kwamba kuna tetesi zinazodai nyota huyo atajiunga na klabu ya Manchester United.

Chelsea wanatarajiwa kuzipiku beat Manchester City na Arsenal kwenye vita ya kusaka saini ya nyota wa klabu ya Hamburg super, Jann-Fiete Arp. (Mirror)

Sam Allardyce amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kazi ya ukocha katika klabu ya West Brom na kusistiza kwamba hana haraka ya kurejea katika kazi hiyo. (Star)

Mshahara wa Neymar kwa mwaka ni sawa na ule wa timu saba bora katika Ligi za wanawake, utafiti ukitaja jambo hilo kama matumizi mabaya ya fedha.

Thomas Lemar
Arsenal watajaribu kumsajili nyota wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar mwezi Januari, lakini ofa yao inategemewa kuwa chini ya paundi milioni 90 walizotoa mwezi Agosti. (Daily Mail)

Meneja wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino amekata tamaa ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza baada ya mechi 13 tu. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 26 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 26 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/26/2017 04:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.