Loading...

Utabiri wa Michael Owen, Liverpool Vs Chelsea

Liverpool watacheza dhidi ya Chelsea katika dimba la Anfield Jumamosi jioni
Michael Owen anawapatia nafasi kubwa vijana wa Jurgen Klopp kushinda mechi yao dhidi ya Chelsea katika dimba la Anfield Jumamosi jioni.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza wameshinda michezo yao minne ya mwisho katika ligi hiyo, ikiwa ni dhidi ya Bournemouth, Watford, Manchester United na West Brom.

Liverpool walifanikiwa kujikusanyia kiasi cha pointi nne katika michezo yao ya mwisho waliyocheza dhidi ya Chelsea msimu uliopita, walianza kwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 Stamford Bridge kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 Anfield.

Shujaa huyo wa klabu ya Liverpool anaamini kwamba, klabu yake ya zamani itaibuka kidedea katika mechi yao dhidi ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Michael Owen
Kwa mujibu wa taarifa ya BetVictor, Owen alisema: “Mchezo kati ya pande mbili ambazo ziko kwenye kiwango cha hali ya juu, pamoja na falsafa za makocha wa pande zote na uwezo wa safu za ushambuliaji ni vigumu kwa kuamalizika kwa sare ya bao 0-0.”

“Pande zote mbili zimefanikiwa zimefanikiwa kufunga katika mechi 11 kati ya 12 na sitegemei kuona mabadiliko katika mwenendo huo kwenye dimba la Anfield.

“Liverpool walikubali kupoteza uongozi wa mabao matatu mbele ya Sevilla katikati ya wiki hii kwenye Ligi ya Mabingwa, lakini wanaonyesha nia ya ajabu kutaka kusonga mbele na nina imani wataishangaza Chelsea.”
Utabiri wa Michael Owen, Liverpool Vs Chelsea Utabiri wa Michael Owen, Liverpool Vs Chelsea Reviewed by Zero Degree on 11/24/2017 05:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.