Loading...

Utafiti: Ziwa Victoria lipo hatarini kukauka

Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka.

Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa.

Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini.

Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, jeshi la Uganda linadaiwa kuweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo zote za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.
Utafiti: Ziwa Victoria lipo hatarini kukauka Utafiti: Ziwa Victoria lipo hatarini kukauka Reviewed by Zero Degree on 11/27/2017 04:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.