Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 27 Novemba, 2017

Robert Lewandowski
Mke wa Robert Lewandowski, ameashiria kwamba mshambuliaji huyo wa Timu ya Taifa ya Poland na Bayern Munich ana mpango wa kutimkia LA Galaxy.

Pep Guardiola anafanya mipango ya kumsajili beki wa klabu ya Real Sociedad, Inigo Martinez. (Sun)

Jurgen Klopp anasema ataondoka Liverpool kabla ya klabu hiyo haijafikiria kumwondoa.

Ben Foster ameunga mkono uamuzi wa klabu ya West Brom kumfukuza kazi meneja wao, Tony Pulis.

Antonio Conte ameiambia bodi ya Chelsea kuhakikisha inakamilisha dili zote za usajili mwezi Januari, iwapo wanataka kuendelea kuwafukuza viongozi wa Ligi kuu, Manchester City.

Baada ya sare na West brom, kiungo wa klabu ya Tottenham, Eric Dier ametupa lawama zote kwa aliyekuwa mwamuzi wa mchezo huo.

Romelu Lukaku anaweza kuikosa mechi ya Manchester United dhidi ya Arsenal kwa sababu ya kufungiwa.

Mwamuzi mstaa, Graham Poll anasema kwamba, Romelu Lukaku anatakiwa kufungiwa kwa kitendo alichokifanya wikendi. (Daily Mail)

Neymar
Mshahara anaolipwa mshambuliaji wa Paris St-Germain, Neymar ni mkubwa zaidi katika msimu mmoja kuliko za wachezaji wote wanaocheza ligi saba bora za wanawake duniani kwa pamoja. (Guardian)

Klabu ya Barcelona inatarajiwa kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark, Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 25, itakapofika mwezi Januari. (Don Balon).

Nahodha wa klabu ya Tottenham, Hugo Lloris amewaomba wachezaji wenzake waache uzembe.

Meneja wa klabu ya Newcastle, Rafa Benitez amewataka mashabiki wa timu yake kuwa na subira baada ya klabu hiyo kushindwa mechi ya nne mfululizo walipochapwa goli 3-0 na Watford wikendi.

Wilfried Bony ameapa kurejea katika kiwango bora na ainusuru klabu yake ya Swansea isishuke daraja. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial
Klabu ya Real Madrid ina mpango wa kuwasilisha ofa ya paundi milioni 80 kumnasa mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial katika majira ya joto mwakani.

Wakala wa kiungo wa kati wa Serbia, anayechezea klabu ya Liverpool Marko Grujic, amesema mteja wake ataondoka Anfield kwa mkopo mwezi Januari kwa sharti kwamba hatatoka nje ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Tottenham wanamfuatilia beki wa kushoto wa klabu ya Bologna, Adam Masina, ambaye anategemewa kuja kujaza nafasi ya Danny Rose, endapo ataondoka mwezi Januari. (Mirror)

Alan Pardew ana karibia kuteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya West Bromwich Albion.

Mshambuliaji wa klabu ya Watford, Andre Gray anasema kwamba timu yake haikuwa bora licha ya kuitandika Newcastle goli 3-0.

Gareth Bale
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa winga wa klabu hiyo na  Timu ya Taifa ya Wales, Gareth Bale hatauzwa wakati wa dirisha ndogo mwezi Januari. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 27 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 27 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/27/2017 04:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.