Loading...

Alichosema Alberto Msando kuhusu wapinzani kwenye mkutano mkuu wa UVCCM

Wakili msomi wa kujitegemea, Alberto Msando
Aliyewahi kuwa mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo na Wakili msomi wa kujitegemea, Alberto Msando amesema vyama vya upinzani nchini vimekosa nguvu katika kupambana na rushwa ukilinganisha na chama tawala cha CCM.

Msando amesema hayo leo tarehe 10 Desemba 2017, mjini Dodoma kwenye mkutano mkuu wa UVCCM taifa uliohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli.

“Wapinzani siyo tu wanapotezana, bali hadi sasa wameshapotezana, tumeshawapiga 4-0 ugenini na tukirudi nyumbani nako ni 4-0, tunamaliza kazi, CCM Oyee!!” – Alberto Msando

Alberto Msando ni moja ya watu mashuhuri saba waliohamia CCM kutoka kwenye vyama vya upinzani.
Alichosema Alberto Msando kuhusu wapinzani kwenye mkutano mkuu wa UVCCM Alichosema Alberto Msando kuhusu wapinzani kwenye mkutano mkuu wa UVCCM Reviewed by Zero Degree on 12/10/2017 04:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.