Loading...

Babu Seya, Papi Kocha waachiwa huru

Babu Seya, Papi Kocha waachiwa huru
Rais John Magufuli leo Jumamosi ametoa msamaha mwanamuziki Nguza Viking pamoja mtoto wake wake Papi Kocha waliokuwa wakitumikia kifungo cha maisha kwa makosa ya kuwanajisi watoto.

Rais Magufuli ametoa msamaha huo wakati akihutubia maadhimisho ya shehere za Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika mjini Dodoma leo.

Familia hiyo imekaa jela tangu ilipohukumiwa adhabu hiyo Juni 5, 2004.

Rais Dkt John Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa wa kunyongwa na wale waliohukumiwa kukaa jela maisha
Rais John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa la Tanzania pia amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake.

Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha
Babu Seya, Papi Kocha waachiwa huru Babu Seya, Papi Kocha waachiwa huru Reviewed by Zero Degree on 12/09/2017 12:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.