Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 9 Decemba, 2017

Hazard na Antonio Conte
Antonio Conte amemwambia Eden Hazard atafute "moto mtakatifu" ndani yake ili kuwafikia akina Cristiano ­Ronaldo, Lionel Messi na Neymar.

Meneja wa Stoke City, Mark Hughes anasema kwamba nafasi ya klabu ya Tottenham kushinda ubingwa inaweza kuwa imeshafungwa tayari.

Wachezaji wa Arsenal walihoji juu ya mbinu za Arsene Wenger katika uwanja wa mazoezi baada ya kupoteza mechi yao dhidi ya Manchester United. (Mirror)

Arsenal hawajampa Jack Wilshere ofa ya mkataba mpya pamoja na kwamba kiungo huyo anaingia katika miezi sita ya mwisho ya mkataba wake wa sasa.

Kuelekea mechi yao ya Jumapili, meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kwamba wachezaji wa Manchester City wana tabia ya kujiangusha.

Jurgen Klopp akimpongeza Coutinho
Georginio Wijnaldum anasema Jurgen Klopp ameirudisha Liverpool mstarini kwa kuwafanya wachezaji wake wawe na morali ya kuichakaza klabu ya Tottenham goli 4-1. (Daily Mail)

Roy Hodgson amemwambi Eddie Howe asichukulie kutazamiwa kuja kuwa meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza kama mzigo kwake bali kama heshima kubwa.

Alan Pardew amemtaka Salomon Rondon aanze kufunga magoli ya kutosha ili amshawishi asisajili mshambuliaji mwingine kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Paul Clement amekanusha taarifa zinazodai kwamba amebakiwa na mchezo mmoja kabla ya kutimuliwa na klabu ya Swansea.

Marco Silva amemtaka Andre Gray kujiweka sawa kwa ajili ya klabu ya Watford akirejea katika klabu ya zamani, Burnley.

Riyad Mahrez
Meneja wa Leicester, Claude Puel anasema kwamba Riyad Mahrez anatakiwa asiruhusu mawazo ya kuwaniwa na vilabu mbali mbali yaathiri kiwango chake tena.

Mauricio Pellegrino amemuonya mshambuliaji wa Southampton, Charlie Austin kwamba anatakiwa kuwa mnyenyekevu na asiwe na kiburi kwa kiwango chake cha sasa. (Star)

Mauricio Pochettino anasema kwamba Tottenham lazima wawe makini na mipango yao ya usajili baada ya kukamilisha mipango yao kwa kuchelewa katika dirisha la usajili lililopita. (Guardian)

Beki wa klabu ya Everton, Jonjoe Kenny anasema kwamba kuifunga klabu ya Liverpool itakuwa ni zaidi ya kubeba Kombe la Dunia.

Rafa Benitez amemuonya Mike Ashley kwamba, bila kuwekeza katika usajili wa wachezaji katika dirisha dogo la mwezi Januari kunaweza kushusha thamani ya klabu ya Newcastle na timu inaweza kushuka daraja. (Telegraph)

Jose Mourinho amehoji kama Pep Guardiola ataruhusiwa kuvaa utepe wa rangi ya njano kuwapa sapoti wanasiasa wa Catalan waliofungwa jela.

Sam Allardyce amemwambia Wayne Rooney kwamba lazima awe mfano kwa wachezaji wenzake wa Everton kwenye mechi yao dhidi ya klabu ya Liverpool siku ya Jumapili. (Independent)

Derby ya Manchester inaweza kuwa kwenye hatari ya kukumbwa na barafu inayotarajiwa kushuka kesho Jumapili katika mji wa Manchester.

Meneja wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino
Mauricio Pochettino amekataa kuzungumzia uwezekano wa Gareth Bale kurejea Tottenham kuelekea kurejea katika uwanja wao wa White Hart Lane mwaka ujao.

Mmiliki wa klabu ya West Ham, David Sullivan ameizuia klabu kusajili wachezaji wenye umri mkubwa bila kumshirikisha meneja wao David Moyes. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 9 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 9 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/09/2017 12:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.