Loading...

Biashara ya pembe za ndovu yapigwa marufuku China


Sheria iliyopiga marufuku kabisa biashara ya pembe za ndovu, imeanza kutekelezwa Uchina hii leo.

Vikwazo vilianza kufu-atwa katika miezi 12 iliyopita lakini sasa, hairuhusiwi kabisa kwa raia wa Uchina, kununua kitu chochote chenye pembe, ndani na nje ya nchi.

Taarifa ya serikali imesema, mfanyabiashara yeyote, anayejidai kwamba anauza pembe iliyopata kibali cha serikali, atakuwa anadanganya.

Hatua hiyo imechukuliwa na China wakati taifa hilo na nchi nyingine za Bara la Asia zikilalamikiwa na dunia kwa kuwa na soko kubwa la meno ya tembo hivyo kuchochea ujangili katika mbuga za Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliipongeza China kwa uamuzi huo.

“China pamoja na nchi nyingine za Bara la Asia zilikuwa ni sehemu ya soko kubwa la biashara haramu ya meno ya tembo kwa hatua waliyoitangaza tunawapongeza na pia tunaomba nchi nyingine ziige mfano huo wa China,” alisema Nyalandu.

Hata hivyo waziri huyo alisema licha ya maadhimisho hayo, bado hali ya ujangili ni mbaya katika Tanzania.

Alisema Serikali inaandaa kikosi maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na jeshi la Marekani kupata mafunzo ya namna ya kukabiliana na ujangili kwa njia za kisasa.

Hata hivyo alisema Tanzania inaongoza kwa kupokea watalii wengi katika nchi za Afrika Mashariki huku sekta ya utalii ikiliingizia taifa mapato ya Sh bilioni 2 kwa mwaka.
Biashara ya pembe za ndovu yapigwa marufuku China Biashara ya pembe za ndovu yapigwa marufuku China Reviewed by Zero Degree on 12/31/2017 07:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.