Loading...

“Tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao” - Mbowe


Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amewataka Watanzania kuwa tayari kukosolewa na viongozi wa dini kwani ndio wanaoliombea Taifa liwe na amani katika kipindi chote tangu nchi ilipopata Uhuru.

Mbowe ameyasema hayo wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu hali ya kisiasa kwa mwaka 2017, ambapo alisema kila mtu ana mapungufu katika utendaji wake wa kazi hivyo kila mmoja awe tayari kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini.

“Lakini viongozi wetu wa dini wana haki ya kusema, wana wajibu wa kusema, hawa ni watu wanaolea Taifa hili kiroho, huwezi kumshambulia Kakobe kama unamshambulia mtoto mdogo, hawa wana waumini wana followers (wafuasi) na hawa ndio kila siku Rais anasema wamwombee, sasa wanamwombea vipi wakati unawapa masharti?,” alisema Mbowe na kuongeza.

“Sisi wapinzani tunakosolewa, viongozi tuwe na unyenyekevu wa kukubali mawazo tofauti tukisemwa, tusijenge chuki katika jamii, vyama vyetu vyote vinaongozwa na binadamu vinaweza vikakosea, tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao, tukikosea waseme.”
“Tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao” - Mbowe “Tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao” - Mbowe Reviewed by Zero Degree on 12/31/2017 08:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.