Loading...

Charlie Austin afungiwa mechi tatu


Mshambuljia wa Southmpton, Charlie Austin amepigwa marufuku ya mechi tatu na shirikisho la soka la Uingireza (FA) kwa kucheza vibaya.

Austin alimkanyaga usoni golikipa wa Huddersfield, Jonas Lossl wakati wa mechi yao Jumamosi ambapo walitoka sare ya goli 1-1.

Mshambuliaji huyo wa Southampton ambaye ameshaifungia timu yake mabao 6 msimu huu atakosa mechi dhidi ya Tottenham, Manchester United na Crystal Palace.

Pamoja na kufungiwa mechi hizo, Austin alipata jeraha na kuondolewe uwanjani mnamo dakika ya 79.

Meneja wake, Mauricio Pellegrino alisema kuwa jeraha hilo litamweka nje Austin kwa wiki kadhaa.
Charlie Austin afungiwa mechi tatu Charlie Austin afungiwa mechi tatu Reviewed by Zero Degree on 12/25/2017 07:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.