Loading...

DCI afunguka kuhusu Lissu, Ben Sanane na Azory Gwanda

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), CP Robert Boaz
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), CP Robert Boaz amezungumzia kuhusu tukio la kupotea kwa Mwandishi wa gazeti la kila siku la Mwananchi, Azory Gwanda, Mwanaharakati Ben Rabiu Saanane na tukio la kushambuliwa na risasi Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu.

CP Boaz akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama nchini, ameeleza kuwa, Jeshi la Polisi limepokea taarifa za kupotea kwa Mwandishi Azory na kwamba limechukua hatua na zipo taratibu za kiupelelezi zinazoendelea na kuwataka watu kuwa na subira.

Kuhusu kupotea Ben Saanane, CP Boaz amesema Jeshi la Polisi haliwezi kusema kila hatua za kiupelelezi kuhusu tukio hilo kwa kuwa hairuhusiwi kisheria na taratibu za kiupelelezi, lakini amesema upelelezi unaendelea na kutoa rai kwa wananchi wenye taarifa sahihi kuzitoa ili kusaidia Polisi kukamilisha upelelezi.

Vile vile, CP Boaz amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuchukua hatua zenye kuwezesha upatikanaji wa watu waliohusika na tukio la kushambuliwa na risasi Tundu Lissu.

Tukio la kupotea Mwandishi Azory linadaiwa kutokea Novemba 21, wakati tukio la kushambuliwa na risasi Tundu Lissu lilitokea Septemba 7 mwaka huu, huku taarifa za kupotea Mwanaharakati Ben Saanane zilianza kusambaa Novemba 18 mwaka 2016.
DCI afunguka kuhusu Lissu, Ben Sanane na Azory Gwanda DCI afunguka kuhusu Lissu, Ben Sanane na Azory Gwanda Reviewed by Zero Degree on 12/21/2017 03:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.