Loading...

PSG: Hatujakata tamaa kwa Alexis Sanchez


Paris Saint-Germain wanakataa kukata tamaa kwa Alexis Sanchez - licha ya kwamba despite Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa raia huyo wa Chile.

Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Sanchez anaelekea Manchester City kwa dili litakalomfanya alipwe mshahara wa paundi laki 400,000 kwa wiki, vinara hao wa Ligi Kuu wakiwa tayari kusbiria hadi ifike kipindi cha majira ya joto mwakani ambapo atakuwa mchezaji huru.

Sanchez ameweka wazi kuwa anataka kuondoka Arsenal kwa sababu anataka kushinda mataji.

Manchester City walitoa ofa ya paundi milioni 60 kwa ajili ya kumnasa Sanchez mwezi Agosti lakini dili hilo halikufanikiwa kwa sababu Arsenal hawakuweza kumpata mbadala wa nyota huyo kwa wakati.

Klabu hiyo inayonolewa na Pep Guardiola, ina uhakika kwamba inawez kusubiri hadi mwisho wa msimu huu ili kumsajili nyota huyo, ingawa PSG wanabakia kuwa na matamanio makubwa ya kumnasa na wanaweza kutoa ofa mwezi Januari.

Ripoti za nchini Ufaransa zinadai kwamba PSG wamewasiliana na wakala wa Sanchez kuhusiana na uhamisho wa nyota huyo kwenda Parc des Princes.

Kwa mujibu wa taarifa ya Canal Plus, PSG wanatambua kwamba Manchester City wako kwenye nafasi nzuri kufanikiwa kumnasa nyota huyo lakini wanakataa kulikatia tamaa dili hilo.

Wakti huo huo. aliyekuwa nyota wa klabu ya Arsenal, Ian Wright amelitaja sakata la mikataba ya Sanchez na Ozil kama "biashara kichaa".

"Suala hili ni la ajabu sana kwa Arsenal, kwa klabu inayotajwa kuwa ni ya kibiashara kuruhusu wachezaji wawili kama wale kuondoka," alisema Wright alipokuwa akizungumza kwenye  mdaharo wa Sky Sports'.

"Sanchez katika ubora wake ana thamani ya paundi milioni 100. Ozil katika ubora ana thamani ya karibuni paundi milioni 70 hadi 80. Arsenal wanaacha jambo hilo lipite. Ni biashara inayotia hasira kwa upande wa menejimenti ya Arsenal.

"Utawauzaje wachezaji kama wale mwezi Januari kwa paundi milioni 25? Ni kama vile unachekwa."
PSG: Hatujakata tamaa kwa Alexis Sanchez PSG: Hatujakata tamaa kwa Alexis Sanchez Reviewed by Zero Degree on 12/21/2017 01:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.