Loading...

Manchester United kushtukiza usajili wa nyota huyu kutoka Chelsea

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho
Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Mail, Manchester United ina matamanio makubwa ya kumpata winga wa klabu ya Chelsea, Willian, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho kuelekea Old Trafford tangu Jose Mourinho achukue madaraka katika klabu hiyo.

Wakati Mbrazil huyo akiwa tayari kwa jambo lolote Stamford Bridge, kwa upande wake Antonio Conte anaonekana kutokuwa tayari kudhoofisha kikosi chake katikati ya msimu, hasa akipigania kutetea Taji la Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester City ambao wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo.

Antonio Conte na Willian
Willian amekuwa na wakati mgumu kutetea nafasi yake kwenye kikosi cha Chelsea tangu Conte achukue madaraka katika klabu hiyo.

Aliyekuwa nyota wa klabu ya Chelsea, Ray Wilkins amesema kwamba anaona kuna uwezekano mkubwa sana wa kufanikiwa kwa uhamisho wa Willian, hasa kwa sababu ya uwepo wa Jose Mourinho.

“Jose anahitaji sana kumnasa Willian na utakuwa usajili bora kwa Manchester United, lakini ninaomba Mungu Chelsea wasikubali kumwacha aende, alisema Ray Wilkins.
Manchester United kushtukiza usajili wa nyota huyu kutoka Chelsea Manchester United kushtukiza usajili wa nyota huyu kutoka Chelsea Reviewed by Zero Degree on 12/17/2017 12:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.