Loading...

Monaco imetuma onyo kali kwa vilabu vya EPL kuhusu Thomas Lemar

Thomas Lemar
Klabu ya Monaco imetuma ujumbe kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza ambavyo vinawania saini ya Thomas Lemar kuzitaka zitambue kwamba hatakuwa huru kuondoka mwezi Januari.

Chelsea, Arsenal, Manchester City na Liverpool zote zimekuwa zikihusishwa na kutaka kumsajili Mfaransa huyo, lakini inaonekana Monaco hawako tayari kabisa kumwachia aondoke mwezi ujao.

Ripoti zinadai kwamba, Lemar alisema angependelea kujiunga na Liverpool, wakati Arsenal na Chelsea pia zimekuwa zikimfuatilia Mfaransa huyo.

Liverpool wanatazamia kuachana na Daniel Sturridge kitu ambacho kitaweza kutoa nafasi kwa Lemar, wakati Chelsea wakiwa na shauku ya kuongeza nguvu kwenye safu yao ya mbele baada ya Mbelgiji Michy Batshuayi kushindwa kufikia kiwango ambacho klabu hiyo inahitaji.

Hata hivyo, uwezekano wa klabu ya Monaco kukubali kumwachia nyota huyo ni mdogo sana kwa mwezi Januari.

‘Suala la kuuza mchezaji muhimu sio ajenda yetu,’’ alisema makamu wa rais wa Monaco, Vadim Vasilyev.

‘Hatujazungumza na Lemar kuhusu uwezekano wa kuondoka mwezi Januari. ‘‘Timu inataka utulivu. Tumefanikiwa kusimama upya. Sasa sio muda wa kuvunja nguvu tuliyonayo.’’

Monaco waliwaachia wachezaji wengi baada ya kutwaa taji la Ligue one msimu uliopita lakini inaonyesha kwamba hawako tayari kupoteza mchezaji mwingine tena kwa sasa.
Monaco imetuma onyo kali kwa vilabu vya EPL kuhusu Thomas Lemar Monaco imetuma onyo kali kwa vilabu vya EPL kuhusu Thomas Lemar Reviewed by Zero Degree on 12/23/2017 11:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.