Loading...

Tumejipanga vema kuhakikisha watanzania wanaishi kwa amani na utulivu - IGP Sirro


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amefunguka na kuwataka watu wanaofikiria kutaka uharifu waache mara moja kwani wasipofanya hivyo wanaweza kujikuta wameishia gerezani au kukatishwa uhai wao na wakashindwa kusherehekea sikukuu.

Simon Sirro ametoa kauli hiyo mkoani Lindi, alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari mjini hapa. Kamanda Sirro amesema mtu yeyote anayefikiria kufanya vurugu au vitendo vya uhalifu wa namna mbalimbali,ikiwemo wa kutumia siraha ni vema akaacha, vinginevyo anaweza akaishia gerezani au kupoteza maisha kabla ya hata hajashehelekea sikukuu hizo.

"Nasema tumejipanga vema karibu timu zetu zote, zikiwemo za upelelezi, za kiterejensia na timu zetu za operesheni nazo zimejipanga kwa ajili ya doria zikiwemo za helkopta, majini kila mahali kuhakikisha watanzania wanaishi kwa amani na utulivu ndani ya Taifa lao" alisema Sirro.

Aidha Sirro alisema kuwepo kwa amani na utulivu kutawafanya wananchi mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara kutekeleza majukumu yao vizuri katika kujiletea maendeleo ndani ya nchi yao.

Mbali na hilo IGP Sirro, ameonya kwa kusema wale wanaofikiria kutumia siraha waachane mara moja mipango hiyo, kwa kuwa ni vigumu kumkamata mtu aliye na siraha na hivyo kitakachotokea ni ama mmojawapo kukatishwa uhai wake, huku akiwataka waalifu kujiuliza mara mbili kabla ya kuchukuwa siraha kwa lengo la kufanya uhalifu.
Tumejipanga vema kuhakikisha watanzania wanaishi kwa amani na utulivu - IGP Sirro Tumejipanga vema kuhakikisha watanzania wanaishi kwa amani na utulivu - IGP Sirro Reviewed by Zero Degree on 12/23/2017 12:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.