Loading...

Muuza bangi alivyoingia ndani ya gari la Polisi bila kujua


Mtu anayeshukiwa kuwa muuza madawa ya kulevya alijipa krismasi asiyoitaka wakati akiingia kwenye teksi akiwa na karibu misokoto 1000 ya bangi na kugundua kuwa alikuwa ameingi kwenye gari la polisi nchini Denmark.

Polisi nchini Denmak walisema kuwa mwanamume huyo alikuwa akirudi nyumbani wakati alipofanya makosa hayo.

Makosa hayo yalitokea katika eneo la Christiana, wilaya moja ya mji mkuu Copenhagen iliyo maarfu kwa biashara ya madawa ya kulevya.

Polisi wanasema kuwa mwanamume huyo atafunguliwa mashtaka.

Polisi walisema kuwa walifurahi kumuona, kwani alikuwa amebeba misokoto 1,000 ya bangi.

Bangi ni haramu nchini Denmark.

Polisi wamefanya uvamizi mara kadhaa katika wilaya ya Christiana miezi ya hivi karibuni wakiwatafuta wauza madawa ya kulevya.

Source: BBC 
Muuza bangi alivyoingia ndani ya gari la Polisi bila kujua Muuza bangi alivyoingia ndani ya gari la Polisi bila kujua Reviewed by Zero Degree on 12/25/2017 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.