Loading...

Mwanamke akamatwa kwa kosa la kukutwa na gunia la Bangi Jijini Mwanza

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa Mwanamke Asha Jeremiah mwenye umri wa miaka 32, aliyekamatwa kwa kosa la kukutwa na gunia la Bangi atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Msangi amesema Jeshi la Polisi moani humo linaendelea na upepelezi pamoja na msako katika maeneo mbalimbali ya visiwa vya Wilayani Ukerewe na pindi upelelezi utakapokamilika Asha atafikishwa mahakamani.


Asha mkazi wa kisiwa cha Lyegoba, anashikiliwa kwa kosa la kupatikana na Bangi ikiwa kwenye gunia moja lililojaa, maboksi matatu yaliyojaa bhangi na misokoto ya bangi 371, vyote vikikadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu kati ya 35 hadi 50, kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi askari walipokea taarifa kutoka kwa raia wema juu ya uwepo wa mtu anayejihusisha na uuzaji wa bangi katika kisiwa cha Lyegoba na baada ya ufuatiliaji ndipo walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na kiasi hicho cha Bangi.

Aidha DCP Msangi ametoa wito kwa wananchi wa Jiji la Mwanza kuacha kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume cha sheria na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa waharifu.
Mwanamke akamatwa kwa kosa la kukutwa na gunia la Bangi Jijini Mwanza Mwanamke akamatwa kwa kosa la kukutwa na gunia la Bangi Jijini Mwanza Reviewed by Zero Degree on 12/21/2017 03:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.