Loading...

Jamie Carragher aionya Chelsea kuhusu Antonio Conte

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte
Carragher ameinya Chelsea kwamba, itafafanya makosa makubwa kama itamwacha Antonio Conte aondoke.

Jamie Carragher
Aliyekuwa beki wa klabu ya Liverpool, Jamie Carragher ana amini Chelsea watafanya makosa makubwa kuachana na Conte ukilinganisha na mafanikio aliyopatia klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Uingereza hadi hivi sasa.

“Nilisema tangu mwanzoni mwa msimu kabla mechi hazijaanza kwamba, nitashangaa kuona kama ataendelea kuwepo msimu ujao kwa sababu hakuona aibu kuzungumzia kukerwa na mfumo wa usajili katika kipindi cha majira ya joto kilichopita,” Carragher aliimbia Sky Sports.

“Chelsea wana mfumo wa kufanya usajili, sio tu kufuata uamuzi wa meneja. Lakini hilo sio kwa Chelsea peke yake. Nafikiri mameneja wanapaswa kulikubali hilo kwa kiasi flani. Tayari ameshaanza kupiga kelele kuhisiana na anachokitaka mwezi Januari.

“Kusema kweli, sijui suala hilo litafanikiwa kwa kiwango gani pale Chelsea. Klabu ya Chelsea imekuwa na mafanikio makubwa katika suala la kubadilisha wakufunzi, lakini nafikiri kumbadilisha Conte litakuwa kosa kubwa. Nafikiri ni meneja sahihi mwenye uwezo mkubwa lakini nitashangaa sana kuuona akiendelea kuwepo pale msimu ujao.”
Jamie Carragher aionya Chelsea kuhusu Antonio Conte Jamie Carragher aionya Chelsea kuhusu Antonio Conte Reviewed by Zero Degree on 12/21/2017 04:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.