Loading...

Tanzania yazidi kushuka kwenye viwango vya soka duniani


Tanzania imezidi kudidimia kwenye viwango vya soka duniani baada ya kushuka kwa nafasi 5 zaidi kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mwezi Novemba.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na FIFA, inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka 142 mwezi Oktoba, ikiwa imeporomoka kwa nafasi tano kutoka juu.

Kwa Uganda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeendelea kuongoza ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani huku Senegal ikiwa inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 kwenye viwango hivyo vya FIFA.

Kwa upande wa 10 bora, Ujerumani imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.

Tanzania ilifanya vibaya kwenye michuano ya CECAFA nchini Kenya mapema mwezi huu pia kwa mwezi Novemba ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Benin .
Tanzania yazidi kushuka kwenye viwango vya soka duniani Tanzania yazidi kushuka kwenye viwango vya soka duniani Reviewed by Zero Degree on 12/21/2017 04:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.