Loading...

Nafasi ya katambi Bavicha yachukuliwa na Patrick Ole Sosopi

Patrick Ole Sosopi
KAMATI ya Utendaji ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), imemteua Makamu Mwenyekiti Bara wa baraza hilo, Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti wake baada ya Patrobas Katambi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita alisema juzi Kamati ya Utendaji ilikutana kujadili ajenda ya kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza hilo Taifa katika kikao cha dharura. Mwita alisema kwa kuwa Sosopi awali alikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, kamati hiyo pia imemchagua John Pambalu kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bavicha Bara.

Alisema kwa kuzingatia majukumu ya viongozi wakuu wa baraza hilo, kamati imeazimia kuwaelekeza viongozi wapya na waliopo ngazi zote za uongozi ndani ya Bavicha, kuendelea kwa kasi isiyoyumba, kulijenga baraza kwa mujibu wa Katiba ya chama na mwongozo wao.

“Kipindi hiki, Bavicha Taifa inawahimiza viongozi wa vijana wa Chadema na vijana wa Tanzania wasimame kidete kuijenga na kuipigania demokrasia ya nchi yetu katika misingi ya Utawala Bora na Haki za Binadamu kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi,” alisema.

Sosopi alisema Bavicha inaenda kuwa imara zaidi baada ya kuondoka Katambi. Alisema hivi sasa wana kazi ya kutengeneza imani kwa vijana wote wa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 na wanaheshimu uamuzi wa Katambi kwa kuwa ni haki yake kikatiba.
Nafasi ya katambi Bavicha yachukuliwa na Patrick Ole Sosopi Nafasi ya katambi Bavicha yachukuliwa na Patrick Ole Sosopi Reviewed by Zero Degree on 12/03/2017 03:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.